UTENGENEZAJI WA VYAKULA VYA KUKU
MWONGOZO KWA MKULIMA.
Utengenezaji wa vyakula vya Kuku
YALIYOMO
Mwongozo kwa mfugaji
Utangulizi
Jinsi ya kupata virutubisho mbalimbali
Mambo muhimu ya kuzingatia katika kuandaa chakula cha kuku
Hifadhi ya vyakula vilivyochanganywa
Utengenezaji wa vyakula vya kuku kwa ajili ya makundi
mbalimbali
mtama
mchicha
mashudu
dagaa
Ufanisi katika shughuli ya ufugaji wa kuku unategemea mambo mbalimbali kama:
• Ujenzi wa banda bora.
• Uchaguzi wa kuku wazazi wenye sifa nzuri.
• Udhibiti na tiba ya magonjwa mbalimbali.
• Ulishaji bora.
Mwongozo huu unaeleza mambo ya msingi katika kuandaa vyakula vya kuku wa rika
tofauti. Kama mifugo wengine, kuku wanahitaji vyakula vyenye virutubisho vyote
muhimu vinavyohitajika na mwili kama wanga, protini, Madini, mafuta , vitamin na
maji.
Jinsi ya kupata virutubisho mbalimbali
Ili kifaranga awe na afya nzuri na akue upesi anahitaji chakula maalum. Chakula
hicho ni mchanganyiko wa viini lishe mbali mbali. Kila kiini lishe ni lazima kiwe katika
kiwango sahihi kulingana na mahitaji ya mwili wa kifaranga. Viini lishe anavyohitaji
kifaranga ni:
• Wanga • Mafuta
• Protini • Vitamini
• Madini • Maji
Mchanganyiko sahihi wa viini lishe kwa mahitaji ya kifaranga, humwezesha kukarabati
na kujenga mwili (kukua) haraka. Viini lishe tulivyovitaja hapa juu hupatikana katika
aina mbali mbali za viungo ghafi vya chakula cha kuku kama ifuatavyo:
mtama aina tofauti.
karanga
mahindi.
Wanga
Wanga hupatikana katika pumba, chenga au dona ya nafaka kama mahindi au
mtama aina ya serena, lulu n.k.
Vyanzo vya Wanga
Mafuta
Mafuta hupatikana katika mbegu kama karanga au alizeti. Mbegu hizi zikikamuliwa
mashudu yake hubaki na kiasi fulani cha mafuta. Haya hutumika kulishia mifugo
mbali mbali.
alizeti
dagaa
mashudu ya karanga
mashudu
Protini
Kiini lishe hiki hupatikana
katika mashudu ya
karanga au alizeti, dagaa,
damu ya wanyama kama
ng’ombe, mbuzi n.k.Damu hiyo unaweza kuipata machinjioni. Changanya damu mbichi na pumba katika ndoo au chombo chochote kilicho wazi upande mmoja. Vuruga mchanganyiko huo kwa kipande cha mti, halafu fikicha kwa viganja ili kuondoa mabonge. Sambaza mchanganyiko huu juu ya bati halafu anika juani mpaka ukauke kikamilifu.
Tahadhari: Ukiamua kutumia damu katika mchanganyiko wa chakula hakikisha utaitumia mfululizo.Maana kuku wakiaasha izoea ikikosekana huanza tabia ya kudonoana.
Protini hupatikana pia katika unga wa mbegu za jamii ya kunde kama maharage,
kunde, soya n.k.
Madini
Madini aina ‘Calcium’ (tamka kalshium) na fosforasi hupatikana katika unga wa
dagaa na mifupa ya wanyama iliyochomwa na chokaa maalum ya kuku ipatikanayo
katika maduka ya pembejeo za kilimo, chumvi, hata na majivu ya kawaida ya jikoni.
chumvi
unga wa mifupa
Maandalizi ya
unga wa mifupa
Chukua mifupa ya wanyama
hasa ile mirefu (ya miguu na
mingineyo) ichome moto
hadi iive. Utafahamu kuwa
imeiva inapokuwa na rangi
nyeupe mifupa mizuri zaidi
ni ile mirefu yaani ya miguu
na mikono kuliko ile ya kichwa ambayo mara nyingi huwa kama mkaa (ambayo
haifai). Iache ipoe kabisa halafu itwange hadi isagike iwe unga. Hapo inakuwa tayari
kuchangnywa kwenye chakula cha kuku wako.
Vitamini
Vitamini hupatikana katika majani mabichi ya mti
aina ya Lusina, majani ya mpapai, mchicha wa
nyumbani au wa prorini.
Vitamini hupatikana pia katika majani mabichi ya
mimea ya jamii ya mikunde kama marejea na luseni
n.k.ambayo hupendelewa kuliwa na kuku. Unaweza
kukausha mimea hiyo kivulini na kuitwanga katika
kinu au kufi kicha kwa viganja ili kupata unga.
Viungo ghafi tulivyovitaja hapa juu hupatikana
katika vijiji vingi hapa nchini. Kwa hiyo mkulima
unaweza kujitengenezea mwenyewe chakula
kinachofaa kwa ajili ya kuku wako.
Mchicha
Chumvi Unga wa Mifupa
Mambo muhimu ya kuzingatia katika kuandaa chakula
cha kuku
- Upatikanaji wa malighafi kama:- Mahindi mtama, pumba, nk. Kutegemeana na kinachopatikana katika eneo husika.
- Uchaguzi wa malighafi utategemea uwezo wa mfugaji.
- Utengenezaji wa chakula unategemea rika la kuku unaowatengenezea.
- Kiasi au uwingi wa chakula kitakachotengenezwa kitategemea uwezo wa mfugaji kifedha.
- Mali ghafi zinazotumika kutengenezea chakula ziwe zimekauka vizuri ili kuepuka uwezekano wa kuota ukungu ambao ni hatari kwa afya ya kuku.
- Hata kama mali ghafi ni kavu ikaguliwe kuhakikisha kwamba haina ukungu na iwe haijaoza.
Matayarisho
- Andaa aina zote za viungo ghafi zilizo bora katika wingi wa kutosha (uzito). Pumba au dona, mashudu n.k. viwe havikuvunda. Tena viwe safi yaani havikuchanganyika na uchafu wowote bila kushambuliwa na wadudu.
- Tayarisha kopo tupu lenye ujazo wa lita 1 kwa ajili ya kupimia. Mfano wa kopo linalofaa ni lile la Pride, Kimbo au Blue band. Kila kiungo unachotaka kuchanganya pima ujazo wa lita moja ili ujue una uzito gani (waweza kuomba msaada maduka ya jirani wakupimie). Ukiishafahamu hivyo utaweza kupima uzito sahihi wa kuweka kwenye mchanganyika wako. Kwa mfano: Kama lita 1 ya pumba ni nusu kilo, ina maana mahali unapotakiwa kuweka kilo 1 utaweka lita 2 yaani makopo 2 ya lita 1.
- Kama unaandaa kiasi kikubwa cha chakula ni vizuri uwe na mizani ya kutumia kwa ajili ya kuandaa chakula chenye uwiano sahihi. Maana ni rahisi kupoteza hesabu za makopo kama unaandaa chakula kingi.
- Kama mchanganyiko wako wa chakula una dagaa, mahindi au mashudu hakikisha kwamba vitu hivi vinabarazwa mashineni kabla ya kuchanganya (yaani vinavunjwa vunjwa).
- Baraza vyakula hivi upate chembechembe zinazolingana na rika ya kuku unaotaka kulisha chakula unachoandaa.
Utaratibu wa kuchanganya viungo ghafi
Kwanza pima kwa makopo au mizani viungo ghafi vyote vyenye uzito mkubwa
viweke kwenye fungu lake moja na kuvichanganya vizuri. Kwa mfano:
- Unga wa nafaka
- Pumba ya mashudu
- Mashudu ya alizeti
Halafu kwenye fungu la pili changanya vizuri viungo vyenye uzito mdogo kama:
- Unga wa dagaa
- Unga wa mifupa au chokaa
- Chumvi ya jikoni
Kutengeneza chakula cha vifaranga umri wa siku ya kwanza hadi
majuma nane (0-8 wiki)
Aina ya vyakula
Unga wa nafaka kama mahindi au mtama
Pumba za mtama, mahindi, uwele,
Mashudu ya, alizeti, , ufuta karanga au pamba n.k
Unga wa mifupa au chokaa ya kuku
Dagaa au mabaki ya samaki
Chumvi ya jikoni
Virutubisho (Premix)
Jumla
Kiasi (Kilo)
40
27
20
2.25
10
0.5
0.25
100
11
Mwongozo kwa mfugaji
Aina ya malighafi
Mahindi yaliyobarazwa
Mtama
Mihogo
Pumba za mahindi
Pumba laini za mpunga
Pumba za ngano
Mashudu ya alizeti
Mashudu ya pamba
Maharage/kunde zilizosagwa
Kisamvu
Lusina/luseni iliyosagwa
Chokaa
Dagaa/Sangara
Mifupa iliyosagwa
Damu iliyokaushwa
Chumvi ya kawaida
Vitamini/madini (premix)
Jumla
1
45
5
-
15
-
-
15
3
1
-
1
5
6
2.25
-
0.5
0.25
100
2
18
-
20
15
-
15
-
5
5
-
5
6
5
2.25
1
0.5
0.25
100
3
-
27
10
15
-
15
-
-
3.5
4.75
5
4
5
2
5
0.5
0.25
100
4
-
-
40
21
-
10
16
-
1
-
2
5
-
2
3.25
0.5
0.25
100
Kiasi kinachohitajika kutengeneza
michanganyiko mbali mbali ya vyakula
(kilo)
Kutayarisha chakula cha kuku wanaokua (miezi miwili na nusu hadi
miezi 5)
12
Utengenezaji wa vyakula vya Kuku
Namba moja hadi nne katika jedwali hili ni michanganyiko wa vyakula aina 4 tofauti
kwa ajili ya kuku wenye umri uliotajwa hapa juu. Ukihitaji kuandaa chakula cha kuku
hao, chagua mchanganyiko mmoja (kwa safu wima) wenye malighafi zinazopatikana
kwenye eneo lako kwa urahisi na utakazozimudu kifedha.
UTAYARISHAJI CHAKULA CHA KUKU WANAOTAGA (MIEZI 5 HADI MIEZI
18) PAMOJA NA KUKU WAZAZI
Aina ya vyakula Kiasi (kilo)
Chenga za Mahindi 31.5
Mtama 15.0
Pumba ya mahindi 13.0
Mashudu ya Alizeti 20.0
Dagaa 12.0
Chokaa 3.0
Premix 0.25
Chumvi 5.0
Jumla 100
Aina ya vyakula Kiasi (kilo)
Dagaa kilo 12.0
Chenga za mahindi 30.0
Mtama 6.75
Mashudu 20.0
Pumba ya mahindi 23.0
Chumvi 0.25
Chokaa 3.0
Mifupa 5.0
Jumla 100
AU
Vyakula hivi vyote vinafaa kwa kuku watagaji na kuku wazazi. Tofauti kwenye kuku
wazazi ni kuwa wanalishwa kiasi pungufu ili wasinenepe na kushindwa uzalishaji.
Mwongozo uliotolewa, hapa juu ni kwa ajili ya kuandaa kilo 100 za chakula cha kuku,
endapo unataka kutengeneza kilo 500 itabidi kila kilichopo kwenye mchanganyiko
kizidishwe, mara tano ndipo kupata hizo kilo 500.
Endapo mfugaji anataka kukutengeneza chini ya kilo 50 hali kadhalika anatakiwa,
kupunguza/kugawanya hizo kilo 100 kwa mbili hivyo unapata kilo 50 unazohitaji.
Vitu vinavyobarazwa ni Mahindi Dagaa Mashudu na mifupa iliyochomwa ambayo
haijasagwa.
Chakula cha vifaranga kiwe laini zaidi kuliko kile cha kuku wakubwa wanaotaga.
13
Mwongozo kwa mfugaji
Kwa kawaida kuku mmoja mtagaji hula gramu 100 za chakula kwa siku. Wastani wa
mahitaji ya kuku 50 kwa siku ni kilo 5.
Angalizo
Mwongozo huu umeekeze jinsi ya kutengeneza chakula cha kuku kwa rika mbali
mbali. Ikumbukwe kuwa aina ya chokaa inayotumika katika utengenezaji wa chakula
cha kuku ni chokaa maalum inayopatikana kwenya maduka ya pembejeo za mifugo.
Siyo chokaa ya kuchimba chini wala ile itumiwayo kujengea nyumba.
Hifadhi ya vyakula vilivyochanganywa
• Baada ya kuchanganya chakula kijaze kwenye mifuko safi, mikavu isiyokuwa
na takataka za aina yoyote na isiyo toboka.
• Hifadhi magunia yako juu ya matofali yaliyopangwa mabanzi juu yake. Hii ni
kwa ajili ya kuepuka unyevu unaotoka sakafuni ambao unaoweza kuharibu
ubora wa chakula kwa kusababisha ukungu.
• Hakikisha chumba cha kuhifadhia chakula cha kuku kisiruhusu panya
kuingia na paa lisivuje.
• Wakati wa kuandaa chakula, weka kumbukumbu ya gharama zote
zilizotumika katika kuandaa chakula hicho mfano:
- Gharama zote za viungo ghafi.
- Gharama za usafiri wa kwenda kununua visivyo patikana katika
mazingira yako.
- Gharama ya kubaraza viungo ghafi n.k.
- Gharama ya muda wako wote uliotumia kukusanya mali ghafi na
kutengeneza chakula.
• Tunza kumbukukmbu hizi zikusaidie kukadiria bei ya kuuza chakula cha
kuku.
• Katika kupanga bei ya kuuza chakula zingatia gharama ya kukiandaa
ongezea na faida mtakayokubaliana katika kikundi cha wazalishaji wa
chakula.
14
Utengenezaji wa vyakula vya Kuku
KUMBUKA YAFUATAYO UNAPOKUWA UNAANDAA
CHAKULA CHA KUKU
• Tumia mali ghafi zinazopatikana ndani ya
mazingira yako.
• Kumbuka wanakikundi wengine wazalishaji wa
kuku wanategemea sana kupata chakula cha
kuku wao kutoka kwa waandaaji wa chakula.
Hivyo mnatakiwa kuwa makini kutengeneza
chakula chenye ubora unaotakiwa kwa kuku.
• Kutozingatia hili kutaharibu mtiririko mzima
wa uzalishaji. Maana matokeo yake ni kuku
kutaga mayai machache chini ya kiwango
kinachotakiwa. Pia hii itaathiri ukuaji wa vifaraga
na kuku wanaoendelea kukua .Uuzalishaji kwa
jumla utashuka.