SOMO LA 2:
CHANJO NA JINSI YA KUCHANJA
Awali ya yote napenda mtambue kuwa chanjo ni kwa ajili ya kuzuia magonjwa mbalimbali yasiwadhuru kuku wako hivyo hupewa kwa kuku Wenye afya tu ambao sio wagonjwa. Chanjo zipo za aina kuu 2 nazo ni:
_Chanjo zilizo hai /live vaccines_:Hizi ni chanjo zenye virusi Hai kwa ajili ya kinga dhidi ya ugonjwa fulani na ni lazima vifike mwilini vikiwa hivyo hivyo hai.
Sifa kuu ya chanjo hizi ni kuwa kinga yake hukaa kwa muda mfupi mwilini na ndizo chanjo za awali mfano ni chanjo ya Newcastle na gumboro.
_Chanjo zisizo na uhai dead vaccines_:Hizi ni chanjo zenye virusi visivyo na uhai /vimekufa.
Aina za Chanjo kulingana na umri wa kuku
Siku ya 1: MAREK'S /MAHEPE.
Chanjo hii hupewa kifaranga wa siku 1mara tu ya kuanguliwa na kinga hudumu kwa maisha yake yote, mara nyingi hutolewa hatchery kwenye makampuni yanayototolesha vifaranga ingawa baadhi ya makampuni hudanganya wafugaji kuwa wamechanjwa wakati hawakuchanjwa ila kwa kujiridhisha zaidi na uwe na uhakika na vifaranga wako unaweza kuchanja mwenyewe, wasipochanjwa siku ya 1 basi unaweza kuwachanja siku ya 18.
_Namna ya kuchanja_: Ni chanjo ya sindano hivyo ni vyema achanje mtaalamu anayejua.
Siku ya 7:NEWCASTLE +IB VACCINE: IB Ni Infectious Bronchitis (chanjo ya mafua) Hii ni chanjo iliyo kwenye chupa 1 lakini ina kinga ya magonjwa 2 ndani yaani Newcastle na mafua. Hii huwa ipo ukiikosa basi utanunua hiyo ya kawaida yenye kinga 1 tu ya Newcastle.
_Jinsi ya kuwapa_: huchanganywa na maji.
Siku ya 14 Gumboro.
Kwa kuku wa kienyeji chanjo hii huwa si lazima kupewa kwani wao huwa wanatotolewa wakiwa na kiasi cha hii kinga.
_Jinsi ya kuwapa_: huchanganywa na maji.
Siku ya 21. Rudia chanjo ya siku ya 7.
Siku ya 28: Rudia chanjo ya siku ya 14.
_Baada ya siku hizi 28 mwezi sasa utakuwa umekwisha na chanjo za awali utakuwa umezitimiza sasa zitafuata chanjo nyingine nazo ni hizi zifuatazo_:
Wiki ya 6: Chanjo ya Ndui /fowl pox:
_Namna ya kuwapa_: Chanjo hii ni vyema ikatolewa na mtaalamu anayejua kwani ni ya kuchanganywa kwanza na kuchoma kwenye mbawa (wing web) na kitendo hichi hufanywa kwenye kivuli pasipo na joto kali kwani hivi navyo ni virus hai.
Wiki ya 8: Chanjo ya typhoid.
_Namna ya kutoa_:Hii nayo hutakiwa kutolewa na mtaalamu anayejua kwani nayo ni ya sindano huchomwa kwenye msuli /muscles.
Baada ya hapo chanjo muhimu na ambazo zinapatikana kwenye mazingira yetu ya kitanzania ni hizo
_Chanjo za marudio_:
Kila baada ya miezi 3 Rudia chanjo ya 1 au ya 7
KiLa baada ya mwaka 1 rudia chanjo ya wiki ya 6.
_NB Chanjo za kuchanganywa na maji ni lazima maji yawe Safi na salama, tafsiri ya maji Safi na salama ni maji yasiyokuwa na madhara ama Uchafu unaweza kuuona kwa macho ama usioweza kuuona na maji hayo ni maji yaliyochemshwa hivyo maji ya chanjo huchemshwa na kuachwa yapoe na kutulia hatimaye ndio yamiminwe ya kuchanganyia chanjo_.
DOSE YA MAJI YA CHANJO
Kitaalamu kiasi cha maji ya kuchanganywa na chanjo huwa ni 25% au ni sawasawa na 4 yaani ni tafsiri ya 25%.
NI KILE KIASI CHA MAJI WANACHOKUNYWA KUKU WAKO KWA SIKU UNAGAWANYA KWA 4
Kwa mfano kuku wangu wanakunywa maji Lita 20 kwa siku nitatafuta 25% ya hayo maji Lita 20 ambayo jibu lake ni maji Lita 5 au njia rahisi unachukua hayo maji Lita 20 unagawa kwa 4 utapata Lita 5, kwa hiyo ntachemsha maji kama Lita 7au 10 niyaweke yapoe ili nije nimimine maji yangu lita 5 ya chanjo.