DAWA ZA ASILI ZA KUTIBU MAGONJWA TOFAUTI YA KUKU

DAWA ZA ASILI ZA KUTIBU MAGONJWA TOFAUTI YA KUKU
Zipo dawa tofauti za asili zinazopatikana kirahisi kwenye mazingira ya vijijini ambazo zina uwezo wa kutibu magonjwa ya kuku. Katika sehemu hii taelezea baadhi ya dawa hizo.
Dawa ya vidonda vinavyotokana na Ndui ya kuku au vidonda vingine vyovyote
Dalili ya Ndui
• Kuku hupata vipele vya mviringo kwenye upanga wake wa kichwani, kwenye masikio, miguuni na kwingineko kusikokuwa na manyoya.

Mmea unaotumika kutibu unaitwa "Shubiri mwitu"

Shubiri mwitu (kiswahili)
Mkankiruri (kinyaturu)
Itembwe (kigogo)
Ibhata (kinyiha)
Litembwetembwe (hehe)
Koli (kikaguru/kinguu)
Aloe (kiingereza)
Aloe vera (kisayansi)

Kuandaa
- Chukua majani ya Shubiri mwitu na kuyachana vipande vidogo vidogo. Vitwange na pumba kidogo na kuvianika.
- Vikiisha kauka vitwange na kuchekecha upate unga laini.
- Hifadhi unga katika chombo kisafi na kikavu.

Kutumia
- Safisha vidonda vilivyotokana na ndui au vidonda vyovyote vile na maji safi yaliyo na chumvi kiasi.
- Pakaa unga wa Shubiri mwitu katika vidonda vilivyosafishwa.
- Rudia baada ya siku moja. Tumia hivyo hadi vidonda vikauke.

Kudhibiti magonjwa mengi mengine ya kuku kwa kutumia Shubiri mwitu ni kama ifuatavyo :
Kuandaa
- Chukua jani moja la Shubiri mwitu lenye ukubwa wa kati.
- Likate katika vipande vidogo vidogo.
- Loweka vipande ulivyokata katika maji kiasi cha lita mbili. Kuku utumia maji haya kunywa yakiwa na vipande hivi vya shubiri mwitu hadi unapobadilisha.

Kutumia
Kuku watumie maji haya kwa kunywa siku zote. Hii inafanya kazi ya kuwakinga kuku dhidi ya magonjwa mbalimbali. Badilisha maji hayo kabla hayajaanza kuchacha na kuwatengenezea dawa nyingine. Hakikisha chombo kinasafishwa vizuri kabla ya kuwawekea dawa nyingine.
#Itaendelea endelea kufatilia
#share_like_comment.
By. Dr. Mpela
http://mpelaaccess.blogspot.com
yohanampela34@gmail.com

Previous
Next Post »