KATIBA
YA
TANZANIA
AGRO INVESTMENTS.
YALIYOMO UKURASA
1. JINA, MALENGO NA DIRA YA KIKUNDI…………………………………………….. 2
2. SIFA ZA KUJIUNGA, MASHARTI, WAJIBU,
HAKI YA MWANACHAMA NA MCHANGO MBALIMBALI………………………... 3
3. KUKOMA UANACHAMA NA HAKI ZA MWANACHAMA ALIYEKOMA…. 4
4. UONGOZI WA KIKUNDI NA UCHAGUZI WA UONGOZI…...………………. 5
5. KAMATI KUU NA MAJUKUMU………………………………………………... 5
6. FAINI NA ADHABU MBALIMBALI……………………………………………. 7
7. MIIKO YA UONGOZI NA UCHAGUZI MKUU…………………………….…... 8
8. MALI NA KINGA ZA KIKUNDI……………………………………………….... 9
TANZANIA AGRO INVESTMENT
KATIBA YA KIKUNDI CHA TANZANIA AGRO INVESTMENT
UTANGULIZI
Kikundi cha TANZANIA AGRO INVESTMENT Kimeanzishwa mnamo 18/09/2017 kama wazo kwa ajili ya kuendesha shughuli za kiuchumi.
1: IBARA YA KWANZA
JINA, MALENGO NA DIRA YA KIKUNDI
A: JINA LA KIKUNDI
Jina la kikundi ni TANZANIA AGRO INVESTMENT.
Makao makuu ya kikundi DAR ES SALAAM.
B: MADHUMUNI YA KIKUNDI
(MISSION)
Kufanya biashara ya ufugaji, kilimo & huduma za kijamii na bidhaa.
Kugawana mapato yatokanayo na biashara
Kuanzisha na kutunisha mfuko kupitia michango ya wanachama na mapato ya biashara.
Kuboresha hali ya kiuchumi ya kila mwanakikundi.
Kusaidiana & kushirikiana kwenye kutafuta masoko na kuendeleza biashara za pamoja na binafsi
C: DIRA (VISION)
Kubuni na kuanzisha miradi ya maendeleo kwa wanakikundi na jamii kwa ujumla
Kukopa pesa katika taasisi mbalimbali za fedha, ili kukipa kikundi uwezo wa kuwekeza katika miradi mikubwa zaidi
2: IBARA YA PILI
SIFA ZA KUJIUNGA, MASHARTI, WAJIBU, HAKI YA MWANACHAMA NA MCHANGO MBALIMBALI
A: SIFA ZA KUJIUNGA
Awe na umri kuanzia miaka 18
Awe na akili timamu
Awe tayari kutimiza matakwa ya cha 2(b)
B: MASHARTI YA MWANACHAMA
Mwanachama achangie michango na malipo yoyote ya kikundi kulingana na katiba.
Mwanachama awe mkweli na mwaminifu
Mwanachama lazima ashirikiane kikamilifu na wenzake katika shughuli za kikundi
Hakuna pesa itakayorudishwa kwa mwanachama akijitoa au kufukuzwa.
Mwanachama anaweza kujitoa wakati wowote.
Mwanachama atoe taarifa kwa tukio lolote ambayo linahusiana na shughuli za kikundi.
C: MICHANGO MBALIMBALI
Michango ya gharama za vikao i.e viti, ukumbi n.k.
Mtaji wa kuanzia biashara kama ada ya kujiunga, kiwango cha chini kikiwa shilingi laki tatu (300,000) na kutokea hapo atapata haki ipasavyo kama mwanachama.
D: WAJIBU WA MWANACHAMA
Kuwa mkweli, muwazi na mwaminifu. Ashiriki katika vikao na shughuli za kikundi.
Kuhudhuria mikutano yote.
Kukubali kukosolewa na kujikosoa kwa maslahi ya kikundi.
Kutekeleza maazimio ya kikao.
Mwanachama haruhusiwi kutoa taarifa za kikundi ambazo zitaathiri maslahi ya kikundi.
Kusimamia maslahi ya kikundi.
E: HAKI ZA MWANACHAMA
Kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi.
Kujitoa uanachama kulingana na mwongozo wa katiba.
Kukosoa na kukosolewa, kushiriki vikao, kutoa maoni.
Kupata haki zote kulingana na mwongozo wa katiba.
Haki ya kupatiwa taarifa sahihi za kikundi na kwa wakati.
Kupata ushuri stahiki kutoka kwenye kikundi.
3: IBARA YA TATU
KUKOMA UANACHAMA NA HAKI ZA MWANACHAMA ALIYEKOMA
A: KUKOMA UANACHAMA WA KIKUNDI
Mambo yanayopelekea kukoma uanachama wa Tanzania Agro Investiment ni kama yafuatayo:
Mwanachama akifariki.
Mwanachama akipenda kujitoa mwenyewe.
Mwanachama atakoma uanachama endapo hatalipa michango iliyoainisha kwa muda wa mwaka mnzima pasipo sababu maalumu iliyowasilishwa kwa uongozi.
Mwanachama atakoma uanachama endapo hatohudhuria vikao vya wanachama vinavyotambulika kikatiba mara tatu mfululizo (kwa wajumbe walioko Dar).
Mwanachama atakoma uanachama endapo atafanya hujuma kwa namna yeyote ile kwa kikundi.
Uongozi unaweza kumvua uanachama au kiongozi uanachama wa kikundi pale itakapo onekana ipo haja au sababu ya kufanya hivyo.
B: HAKI ZA WANACHAMA ALIYEKOMA
TANZANIA AGRO INVESTMENT ikiwa kama kikundi chenye weledi, siku zote itasimia haki za wanakikundi, Iwapo mtu yeyote atakoma uanachama kutokana na sababu zilizoainishwa katika ibara ya 3 (a) atapatiwa haki zake kama ilivyoainishwa hapo chini:
ALIYEFUKUZWA –Atapata haki zote (gawio) kwa asilimia arobaini (40%). Haki hii ataipata miezi mitatu baada ya kukoma uanachama.
ALIYEJITOA –Atapewa haki zake (gawio) kwa asilimia arobaini (40%). Haki hii pia italipwa miezi mitatu baada ya mwanachama kuwasilisha barua yake ya kuomba kujitoa kwa uongozi wa kikundi.
KIFO, MATATIZO YA AKILI AU KIJITOA KWA MARADHI YA MUDA MREFU-Atalipwa haki zake (gawio) kwa asilimia mia moja (100%).
Haki hii itakabidhiwa kwa warithi wa mwanachama kama alivyowaainisha katika fomu ya kujiunga na kikundi. (fomu ya kukokotoa haya malipo itawekwa wazi)
4: IBARA YA NNE
UONGOZI WA KIKUNDI NA UCHAGUZI WA VIONGOZI
A: UONGOZI WA KIKUNDI
Kikundi kitakuwa na viongozi wafuatao ambao watachaguliwa na mkutano mkuu wa wanakikundi kilichotimia koramu ambayo itakuwa kinaitishwa na kamati ya uchaguzi kupitia mwenyekiti wake. Viongozi wafuatao ndio watakaounda uongozi mzima wa kikundi:
Mwenyekiti
Katibu & Muweka hazina
B: UCHAGUZI WA VIONGOZI
Kiongozi atachaguliwa endapo koramu itavuka nusu ya wanakikundi wote.
Uchaguzi wa kiongozi utafanyika kila baada ya mwaka.
Viongozi watapatikana kwa njia ya kupendekezwa au na kura.
5: IBARA YA TANO
KAMATI KUU NA MAJUKUMU
A: Kamati hii inaundwa na:
Mwenyekiti
Katibu
Muweka Hazina
NB: Kutaundwa KAMATI nyingine ndogo kutokana na uhitaji
UPATIKANAJI
M/kiti na katibu wanapatikana kwa njia ya kuteuliwa na kuchaguliwa kulingana na ibara ya 4(b)
B: MAJUKUMU YA M/KITI
Kusimamia shughuli zote za kamati kuu na kikundi kwa ujumla.
Kupitia, kukosoa, kuboresha ( kama kuna ulazima) na kutoa mapendekezo/maamuzi juu ya ripoti za kamati.
Kusimamia haki, sera na katiba ya TANZANIA AGRO INVESTIMENT, katika kutoa maamuzi bila kutegemea upande wowote.
C: MAJUKUMU YA KATIBU WA KAMATI KUU
Kumshauri m/kiti juu ya mambo mbalimbali yanayohusu kamati kuu.
Kuandaa muktasari, ripoti na agenda za kamati kuu baada / kabla ya mkutano.
Kusimamia majukumu ya m/kiti iwapo m/kit hayupo.
Kufanya kazi yoyote atakayoelekezwa na m/kiti kulingana na katiba ya TANZNIA AGRO INVESTIMENT.
D: MAJUKUMU YA KAMATI KUU
Kamati hii ndio itakua inasimamia kamati zingine kwa kutoa ushauri, maelekezo, kukosoa na nk.
Kupokea ripoti na mapendekezo (B’ness plan/Idea/Projects) Kutoka kwa kamati mbalimbali na kushauri, kukosoa, kuboresha (kama kuna hoja) kabla haijawasilisha kwa wajumbe kwa masuala ya uwekezaji, rufaa nidhamu na nk.
Kuunganisha kamati zingine / kiungo katika zingine katika taarifa, ushauri, maamuzi nk. (trend in judgment)
Kupokea ripoti mbalimbali kutoka kila kamati eg Ripoti ya mapato na matumizi, uwekezaji nk.
Kuitisha mkutano mkuu kulingana na mwongozo wa katiba au itakapohitajika kufanyika hivyo (Agenda uchaguzi mkuu, kusitisha uanachama kwa mwanachama, kifo cha kiongozi au mwanachama)
M/kiti wa TANZANIA AGRO INVESTIMENT ndio ana haki ya kuitisha mkutano mkuu/ mkutano mkuu wa dharura.
6: IBARA YA SITA
A: FAINI NA ADHABU MBALIMBALI
ADHABU ZOTE KWA MAKOSA YATAKAYOFANYIKA NA MWANACHAMA, KAMATI KUU ITASIMAMIA NA KUPANGA KWA MUHUSIKA KWA MUJIBU WA KATIKA.
Pesa zote za faini zitakusanywa na kiongozi na zitawakilishwa kwa mweka hazina kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo ya TANZANIA AGO INVESTMENT.
Mwanachama atayechelewa saa moja baada ya kikao kuanza atatakiwa kulipa sh. 2000/ kama faini.
Mwanachama ambaye hataudhulia kikao bila sababu za msingi/ kutotoa taarifa mapema kwenye uongozi siku moja kabla ya kikao atatakiwa kulipa faini ya sh. 5000/
Mwanachama atakayekosa kuhudhulia vikao vitatu mfululizo bila taarifa atavuliwa uanachama (exceptional kwa walio nje ya DSM).
Mwanachama ambaye atatoa siri/documents za kikundi, atavuliwwa uanachama.
NB: Faini (i) na (ii) zitakazotolewa zitagharamia kikao husika.
7: IBARA YA SABA
MIIKO YA UONGOZI NA UCHAGUZI MKUU
A: MIIKO YA UONGOZI
Kiongozi aogope na kuepusha ubadilifu wa mali za kikundi, Kiongozi yeyote atakaebainika amefanya ubadilifu atashitakiwa kwa mujibu wa sheria.
Kiongozi asitumie dhamana ya uongozi kwa upendeleo.
Kiongozi awe na upendo na moyo wa kujituma.
Kiongozi akilalamikiwa na wanakikundi, wanakikundi wanauwezo wa kumtoa madarakani endapo malalamiko yakidhibitika na kamati kuu.
Kiongozi atoe taarifa ya mgawanyo/mgongano wa maslahi kati ya kikundi na uongozi.
B: UCHAGUZI MKUU
Kamati kuu ndio inayoandaa uchaguzi mkuu, kamati kuu pia ndio inayoandaa agenda na kusimamia uchaguzi mkuu, Uchaguzi mkuu unafanyika mara moja kwa mwaka kila mwezi December (uteuzi).
Uchaguzi huu utahusisha viongozi wa juu wa TANZANIA AGRO INVESTIMENT.
Endapo kiongozi atafariki, kufukuzwa na kujiuzuru kamati kuu itaitisha mkutano mkuu wa dharura na kufanya uchaguzi ili kupata kiongozi mpya atakaemalizia kipindi cha uongozi kilichobakia (uteuzi).
8: IBARA YA NANE
MALI NA KINGA ZA KIKUNDI
A: MALI ZA KIKUNDI
AKAUNTI YA HUNDI iliyopo CRDB/ NMB BANK tawi la ……. Account namba …………………………………………
B: KINGA ZA KIKUNDI
Katiba ya TANZANIA AGRO INVESTMENT inanguvu kisheria na inaweza kumshitaki mwanachama wa TANZANIA AGRO INVESTMENT asiye mwanachama wa TANZANIA AGRO INVESTMENT kulingana na sheria/ Katiba ya TANZANIA AGRO INVESTMENT na kama ikihitajika sheria ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inaweza kutumika.