MpelaAccessTz1.com
Prepared by Dr. Mpela
KILIMO CHA MATANGO.
Tunda linalostawi maeneo ya kitropiki na lenye faida kemkem za kiafya ikiwemo upatikanaji na vitamin A pamoja na waswahili husema ulaji wa tunda hili husafisha figo, na huku wataalamu wakieleza tunda hili Husaidia katika kuongeza maji mwilini, pia Husaidia katika mmeng`enyo wa chakula.
Mikoa mingi hapa Tanzania huzalisha zao hili kwa wingi, ikiwemo Arusha, Tanga, Tabora, Mwanza, Pwani, Morogoro na mingine mingi.
HALI YA HEWA.
Joto liwe 18 hadi 35 setrigrade, mvua iliyo ya wastani, umbali kutoka usawa wa bahari ni mita 1000 – 1200.mvua ziwe za wastani.
kwa kilimo cha matango suala la kuzingatia ni kuhakikisha unapanda mbegu bora na unafuata kanuni zingine za kilimo, ikiwemo kuzingatia uandaaji wa shamba kwa kusafisha na kuondoa kila aina ya uchafu uliopo pia kuandaa matuta yenye muinuko na kuweka mashimo katika vipimo vinavyotakiwa, upandaji wa nafasi, palizi, uzuaji wadudu wasumbufu kama inzi weupe, usegekaji (staking), kuvuna kwa wakati. Usipande matango sehemu zenye mwanga mkali au sehemu ambazo zenye kivuli, hivyo matango yapandwe katika sehemu zenye mwanga wa kutosha na sio uliozidi au kupungua, kwa kuzidi kwa mwanga matango hupelekea maua dume kuzaliwa kwa wingi, na kwa kupanda sehemu zisizo za mwanga hupelekea maua ya kike kuzaliwa kwa wingi, pia ukuaji duni pamoja na magonjwa ya fangasi.
Hili kuziia mwanga kuzidi au kupungua kilimo cha greenhouse kimefanikisha hili suala la mwanga, mbali na hapo waweza tumia nailoni maalumu kwa suala la mwanga.
MAANDALIZI YA SHAMBA.
Kabla ya kuandaa shamba chagua sehemu ya kuweka shamba lako la matango, shamba liwe na udongo tifutifu udongo ambao unapitisha maji, udongo wenye rutuba, wenye chachu ya udongo (soil pH) 5.5 hadi 6.5. sehemu pia mzungo wa hewa uwe wa kutosha.
Shamba liwe sehemu inayofikika kwa urahisi pamoja na hayo shamba liwe karibu na barabara kuu ambayo itarahisiha usafifrishaji kutoka shambani kwenda sokoni.
USEGEKAJI (STAKING).
Weka miti (nguzo) katika kila shimo lenye mche kwa lengo la kuuweka mmea kuwa imara na matunda kuwa yenye ubora kwa kuacha matunda kuwa chini hupelekea matunda kuoza na wadudu kutoboa.
Miti hii iwekwe ikiwa na mtindo wa matawi na usiwe mti wenye kunyooka kama inavyotumika katika nyanya.
AINA ZA MATANGO.
Zipo aina nyingi za matango ambazo huzalishwa hapa nchini zikiwemo, Colorad, Telegraph, Palmetto, Chicago, Pickling, Straight 8 na Marketer.
UPANDAJI.
- Ni vizuri ukapanda mbegu za matango moja kwa moja shambani na huchukua muda wa siku saba.
- Japo wakulima wengine hupendelea kupanda kwenye vitalu kwanza na baadae kupeleka katika shamba kuu na miche ya matango huamishwa unapofikia urefu wa sentimeta 8 hadi 12.
- Matango hustawi zaidi katika udongo wenye rutuba na unaopitisha maji hapa udongo ni muhimu huwa wa tifutifu.
- Kina cha upandaji ni mita 30.
- Panda mbegu moja katika kila shimo moja.
NAFASI ZA UPANDAJI.
Nafasi kati ya mche na mche nii sentimeta 60 – 70 nafasi kati ya mstari na mstari ni 70 - 90
MATUMIZI YA MBOLEA.
Kwa udongo usiokuwa na rutuba ya kutosha uwekaji wa mbolea ni jambo la msingi kuhakikisha unapata mmea wenye afya.
Kabla ya upandaji andaa shamba lako kwa kuweka mashimo ambayo yatawezesha ukuaji mzuri wa mmea.
Weka samadi itokanayo na wanyama kama ng’ombe, kuku, mbuzi cha kuzingatia mbolea iwe imepoa zaidi ya wiki moja na zaidi, na isiwe ya moto yapaswa kuwa imekaa zaidi ya wiki.
Kwa kutumia mbolea za viwandani (mbolea za chimvi chumvi), tumia mbolea aina ya DAP, NPK. Kwa kupandia tumia mbolea ya NPK na kwa kukuzia tumia DAP.
WADUDU WAHARIBIFU
Wadudu waharibifu katika matango ni
- Inzi weupe (fly fruit).
Wadudu hawa hukaa chini ya majani ya mmea.
Na husababisha majani kusinyaa na kuwa namikunjo.
- Minyoo ya mizizi (nematodes).
Minyoo hii hupeleka kudumaa kwa mmea, minyoo hii huonekana kwa mafundo kwenye mizizi.
- Cucumber Beetle (Tango mende).
Huyu ni mdudu mbaya sana kwa zao hili. Hutafuna miche ya matango na maboga mara ichipuapo, pia hushambulia majani ya mimea michanga
- Melon Aphid.
Hufyonza utomvu wa mimea. Tumia Malathion. Hakisha dawa inafikia upande wa chini wa majani
- Funza.
Buu au funza hujipenyeza ndani ya ua,kisha huhamia kwenye tunda.Tumia Rotenone au Crylite kila baada ya jumla.
MAGONJWA
- Magonjwa ya bacteria.
Majani yaliyoshambuliwa hunyong'onyea na kudhoofu na hatimaye hufa. Mmea ukikatwa huchuruzika ute mzito. Nyunyizia dawa ya Copper kila baada ya siku 10 na tumia aina zenye uvumilivu mkubwa kama vile Palmetto.
- Ubwiri poda (Powdery Mildew).
Ukungu wake hushambulia majani na mashina. Nyunyizia dawa ya unga ya sulphur kila baada ya siku 10.
- Virusi vya wadudu (Cucumber Mosaic)
Husababishwa na sumu (virus). Hali ikiwa mbaya zaidi mmea hugeuka njano, hudumaa na hushindwa kutoa matunda. Huenezwa na magugu au wadudu kama aphids na beetles. Usafi bustanini unahitajika.
- Ukungu (Fog)
Ugonjwa huu husababishwa na hali ya hewa ya ubaridi, na namna ya kuuziana ugonjwa huu ni matumizi ya dawa/sumu maalumu ambazo ni copper fungicide.
- Magonjwa ya virusi (viral disease).
Sehemu athirika ni majani, shina pia huathiri ukuaji wa mmea.
Magonjwa mengi ya virusi huzuiliwa na kupanda mbegu ambazo zinahimili magonjwa.
- Kuoza kwa matunda (Fruit rot)
Kuoza kwa matunda hutokea pale ambapo hutaruhusu matango kutambaa chini na wadudu kushambulia matango kwa urahisi, hivyo uwekaji wa miti katika mashina ya matango kuoza huku kutaepukika.
MATUMIZI YA VIATILIFU.
- Matumizi ya viatilifu yategemee sana hali ya mmea kama imeshambuliwa na magonjwa au wadudu,
- Matumizi ya viatilifu/dawa/sumu kulingana na ushauri wa wataalamu.
KUVUNA
Matango huchukua siku 50 hadi 60 shambani hadi kuwa tayari kuvunwa na matunda yanakuwa na urefu wa sentimeta 15 mpaka 20, makadirio ya mavuno ni Tani 6 kwa ekari moja.
MAMBO YA KUZINGATIA.
Panda kwa wakati, hakikisha unachanzo cha maji ambacho hakita tegemea sana mvua, zuia magugu na magonjwa hii itapelekea mazao yako shambani uwa na uhakika wa kuvuna na kupata faida uanayo itegemea.
Mara baada ya kuvuna kwa wakati hakikisha una osha baada ya kuvuna hili kutoa joto ambalo limetokanalo shamba.
Usipulize dawa/sumu yeyote endapo muda wa kuvuna umekaribia na kama utakuwa umepulizia hakikisha kuwa muda wake mpaka dawa ile hiishe ndio unavuna usipeleke mazao ambayo yana mabaki sumu kwani utahumiza watumiaji wa matunda haya.
Muda unaoshauriwa kuvuna mazao yako ni iwe mapema asubuhi au jioni ya kuanzia saa kumi mpaka pale jua litakapo zama, lengo la kufanya hivi ni kuepuka jua kali kwani upelekea kuharibu ubora wa mazao baada ya kuvuna.
Kwa wanao safirisha kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ambayo ni umbali mrefu usisafirishe wakati wa jua kali safirisha muda ambao ni tulivu na hakuna joto kali au kusafirisha wakati wa usiku, hii itasaidia kuwa na mazao yenye ubora unaoitajika sokoni.
Hakikisha unapeleka mazao yenye ubora na ukubwa kwa lengo la kupata faida nzuri.
http://www.mpelaaccess.blogspot.com
Next
« Prev Post
« Prev Post
Oldest
Post a Comment
Subscribe to:
Post Comments (Atom)