BODI YA SHIRIKA LA RELI (TRL) YAWATAKA WAFANYAKAZI WAKE KUBADILIKA KATIKA UTENDAJI WAO.


Bodi ya shirika la reli nchini (TRL) imewataka wafanyakazi wa shirika hilo kubalika katika utendaji wao, ili shirika liweze kuwa na tija na umuhimu wao wa kuwa wafanyakazi wa shirika hilo uonekane.

Wito huo umetolewa mjini Dodoma na Mwenyekiti wa Bodi ya (TRL) Profesa John Kondoro, wakati yeye pamoja na wajumbe wake wa bodi walipokutana na wafanyakazi wa reli kituo cha Dodoma.

Aidha, Mwenyekiti huyo bodi ya (TRL) amewataka wafanyakazi hao kuwa kitu kimoja katika utekelezaji wa majukumu yao, kwa kuhakikisha shirika hilo linajiendesha kwa ufanisi, kinyume na ilivyo kwa sasa.

Kupitia risala ya wafanyakazi hao, wamedai menejimenti imeshindwa kuwaongeza mishahara pamoja na juhudi walizofanya kufufua mabehewa zaidi 60, ambapo Mkurugenzi Mkuu wa (TRL) Bw. Masanja Kadogosa akawakumbusha juu ya madeni makubwa shirika iliyokuwa nayo na jitihada zilizofanywa kuyalipa madeni hayo.

Previous
Next Post »