VITU VYA KWANZA KUWA NAVYO SHAMBANI KAMA HUDUMA YA KWANZA KWA KUKU.

Watu wengi sana nyumbani hawawezi kosa Dawa kama panadol na kadhalika kwa matumizi yao.

Hivyo kwa kuku yapaswa kuwa na madawa ya huduma ya kwanza.

Nini faida ya kuwa na Madawa ya huduma ya kwanza.

1. Kuwapatia kuku wako ahueni pindi wanasubilia tiba kamili toka kwa Dr

2. Kusaidia kupunguza vifo
Kuna magonjwa ya kuku ndani ya masaa 3 hadi 6 kuku anakufa, hivyo asipo wahiwa kupewa dawa ya huduma ya kwanza ni shida

3. Endapo kuku wameugua weekend ambapo maduka mengi yamefungwa. Weekend kama jumapili unakuta maduka yamefungwa sasa mpaka usubili juma 3 hapo kati kati utapoteza kuku wa kutosha.

VITU MUHIMU.

1. Dawa za antbiotic
Hizi ni za muhimu sana, na zinaweza okoa sana vifo vingi na kuwapa antibiotic hakumanishi mpaka uambiwe, wewe mwe mwenyewe unaweza kujizidisha na kuwapatia ili kuwapunguzia maumivu.

2. Dawa za kuhara hasa ( diarrhea.)
Magonjwa ya kuhara hasa ya mlipuko ni mabaya sana na yanaweza ndani ya masaa kadhaa kuua kuku wako wengi sana sasa fikiria wameanza kuharisha jumapili na maduka yamefungwa.
Kuharisha kuna kwa aina nyingi na kwa sababu nyingi sana hivyo umakini ni mihimu sana

3. Madawa ya kuzuia bakiteria na fangus.
Haya ni kama madawa ya vidonda endapo kuku amepaya jeraha na kuumia anatakiwa kupakwa dawa ya kuzuia bakiteria na pia kupewa antbiotic

4.Dawa za kuboost vitamini.
Kuku wanaweza athiriwa na joto au kitu kingine na with no time wakapata shida so yapaswa kuwa na dawa za vitamini za kuboost na pia kupungiza stress.
Stres pekee huua kuku.

5. Dawa za kuondoa sumu.
Poisoning, kuku wako wanaweza kupata sumu kupitia chakula, Hewa na maji na kuna sumi zingine zinaua faster kiasi kwamba ndani ua masaa 6 hata chini ya hapo unaweza poteza kuku wote.
Hivyo kuwa na dawa ya kuflash sumu ni muhimu sana.

Na dawa zingine utakazo ona zinafaa wewe kuwa nazo.
Kumbuka hii ni huduma ya kwanza na ni kwa.magonjwa ambayo usipo yawahi basi Maangamizi yanaweza kuwa makubwa sana na kupoteza kuku wengi mno ndani ya masaa kadhaa tu.
Unaweza kuwa na kuku 400 baada ya masaa kadhaa tu wakawa wamebakia 60.

Previous
Next Post »