Kimsingi Kuna wakati mwingine ambao umekuwa unatamani kuwa sehemu fulani kwa maana ya kwamba unatamani ndoto yako iwe imetimia lakini umekuwa hujua ni vitu gani ambavyo unatakiwa kuvizingatia ili kuweza kuwa kile ambacho unataka, nakusihi ushushe pumzi kisha twende sawa maana nipo kwa ajili yako.
Yafutayo ni mambo manne (4) ya kuzingatia ili iweze kutimiza ndoto yako.
1. Kuwa na nguvu ya rohoni.
Nguvu ya rohoni katika safari yako ya mafanikio imegawanyika katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ya nguvu ya rohoni amini katika Mungu kwamba mungu yupo hivyo unatakiwa kumuomba kwa imani uliyonayo ili Mungu aweze kukusaidia, pia maisha ya dini yatakufanya uweze kuishi kwa kanuni na sheria zake, pia kama una amini hilo ni lazima ndoto yako itakwenda kuwa kweli maana Mungu ni muweza wa yote, sehemu ya pili ya nguvu ya rohoni ni kwamba ni lazima uweze kujiamini wewe mwenyewe juu ya ndoto yako kwamba inakwenda kutimia.
Mfano unataka kuwa mfanyabiashara wa nguo ukiwa na imani hiyo ni lazima ndoto hiyo iweze kuwa kweli. Imani ndiyo ambayo itakusaidia juu ya jambo lako kwa kuwa utakuwa pia unamini katika nguvu ya Mungu ili kutimiza hilo jambo lako. Pia ikumbukwe ya kwamba nguvu hii ya rohoni itakusaidia kukupa matumaini ambayo yatakusaidia kupambana pia itakusaidia kukipata kile ambacho unakitaka uweze kukipata.
2. Kuwa na malengo.
Kila mtu kwa namna moja ama nyingine ana malengo ila malengo hayo mengi huwa hayatimii kwa sababu mhusika huyo hajui ni namna gani! Unaweza kuyatimiza malengo hayo? Usichoke endelea kufuatana nami mpaka mwisho nitakujuza namna ya kutimiza malengo hayo. Moja ya njia bora ya kutaka kutimiza malengo yako ni lazima uweze kujitambua.
Kujitambua huko ndiko ambako kutakufanya uweze kujua wewe upo vizuri kwenye nini? Kwa mfano baada ya kufanya uchambuzi huo ndipo utapojua kwamba wewe ni mkulima, mwanasisasa, mtangazaji, mshereheshaji na mengine mengi. Baada ya kujua malengo hayo haijalishi ni malengo ya muda mrefu au muda mfupi, ndipo utakapojua kwa undani zaidi kwamba unaelekea wapi. Pia ikumbukwe ya kwamba uwe na malengo ya kitu ambacho anakipenda kwani utakwenda kutenda kitu hicho kwa ufanisi zaidi bila kujali changamoto ambazo zitajitokeza.
3. Kuwa na mikakati.
Baada ya kuwa na malengo ya jambo ambalo unataka kuwa, jambo ambalo linafuata ni kuwa na mikakati, mikakati ambayo itakufanya wewe uweze kufikia malengo yako, ila jambo la msingi la kuzingatia kila mikakati yako ni lazima uiandike katika sehemu ya kumbukumbuka zako ili isiwe rahisi kwako kuisahau. Inawezekana malengo yako yanahitaji kujifunza kwa kusoma hivyo huna budi kusoma, kwa mfano unataka kuwa mwanasheria na hayo ndio malengo yako ni lazima uweze kuwa tayari kujifunza kuhusu sheria.
Pia inawezekana unataka kuwa mfanyabiashara fulani katika eneo fulani mara kadhaa umekuwa ukishauriwa ya kwamba ni lazima ujifunze kwa watu ambao wanafanya vizuri biashara ni kweli fanya hivo kwani hii itakupa matumaini ya kwamba na wewe unaweza. Sio kwa biashara tu bali kwa jambo lolote ambalo unataka kufanikiwa ni lazima ujifunze kwa watu waliofanikiwa. Pia tubakubushwa ya kwamba tusijifunze kwa watu walioshindwa kwani hawawezi kutusaidia zaidi ya kutukatisha tamaa.
Kumbuka kama unataka kuwa mtu fulani kwa hapo baadae ni lazima uanze kuishi ndoto hizo sasa. Mfano unataka kuwa mbunge unatakiwa kuishi maisha hayo sasa japo hujafikia ubunge huo kwa kuangalia wabaunge wanavyofanya sasa na wewe uanze kufanya vivyo hivyo kwa sasa. Pia tunakubushwa ya kwamba kila fursa yeyote ni lazima iwe na maandalizi bora ili kuweza kuwa kile unachotaka. Kuna mwandishi mmoja aliwahi kuandika na kusema hivyo ulivyo leo unatoka na maabdalizi yako ya Jana. Hivyo kuwa na maandalizi leo ya ndoto yako ya kesho.
4. Kuwa na bidii.
Kwa jambo lolote ambalo unalifanya leo na unalitaka liwe matokeo chanya ni lazima ulifanye kwa juhudi na bidii zote. Bidii ambayo itakufanya uweze kutimiza mikakati yako ambayo umejipangia na mikakati hiyo itakusaidia kwa kiwango kikubwa kuweza kutimiza malengo yako.
Pia katika suala la kuwa na bidii katika jambo lako ni lazima uwe chanya, kuwa chanya kunakufanya usiweze kukataa tamaa mapema. Pia tuambiwa kukata tamaa ni dhambi kubwa sana, hasa katika ulimwengu huu usikowa na mwisho hapa nina maana ulimwengu wa mafanikio.
Nafahamu fika ya kwamba inawezekana mara kadhaa kuna watu wamekuwa wakikukatisha tamaa, nakusihii wasikilize watu hao ila maneno yao ya kukukatisha tamaa yafanye kama chachu ya wewe kusonga mbele zaidi.