JINSI YA KUANDAA KILIMO CHA GREEN HOUSE(NYUMBA KITALU)
Green house=Kwa tafasiri isiyo rasmi, ni Nyumba kitalu. Nyuma ambayo imejengwa kukidhi mahitaji mahitaji ya mimea, nyumba hizi hujengwa kwa ustadi mkubwa wa kitaalumu kwa kuzingatia baadhi ya mambo muhimu yakiwemo haya…!
1. Hali ya hewa ya eneo husika (Joto, Baridi, Mwanga wa jua, uelekeo wa upepo, Muinuko kutoka usawa wa bahari, aina ya udongo, ubora wa maji,Mtelemko wa eneo husika)
2. Aina za malighafi za kutumika na ubora wake (Lailoni, net kivuli, mbao au chuma, plastic n,k)
3. Upatikanaji wa maji
4. Kufikika kwa eneo
5. Muinuko wa jengo (Gutter height).
Ni muhimu kuzingatia Urefu/muinuko kutoka usawa wa ardhi kabla ya kuezeka green house.
Mazao yanaooteshwa humo yako ya aina maalumu (kwa maana ya aina ya mbegu za kutumika/Hybrid/F1, zenye sifa mbalimbali kama urefu (kurefuka) ipo namna yake ya uwekaji mbolea, ipo namna yake ya kumwagilia etc ambazo ni njia/namna tofauti sana na inavyofanyika katika open field (Shamba wazi)
A; Kwa nini watu wengi wanawaza/wanaingia katika kilimo hiki?
Taarifa za kuonyesha kilimo hiki hutoa mavuno mengi katika eneo dogo
Zipo taarifa zinaenezwa na watu kuwa unaweza kupata tani 60 za zao kama nyanya ndani ya green house kwa eneo la upana wa mita 8 na urefu wa mita 15).Taarifa kama hizi huwavutia sana watu, kwani mtu hupiga haraka hesabu za mapato na kuona kuwa inalipa (tani 60= kilo 60,000, tufanye kila kilo uiuze tsh 1000, tayari UNA MAPATO YA TSH 60,000,000)
Taarifa za kuonyesha kuwa kilimo hiki hakina usumbufu ni mwendo wa kupata pesa tu.
Zipo taarifa zinasambazwa katika vyombo vya habari, zikionyesha kuwa ukimaliza kujenga tu jengo la green house, basi wewe ni tajiri yaani utakuwa na kazi ya kupanda na kusubiri kuvuna tu hata kwa miaka 10
mfulululizo.
Kwa taarifa kama hizi hufanya mtu kuwaza mapato makubwa, kuwa ikiwa kwa labda miezi 3 tu nina tani 60 za nyanya kwa eneo la mraba la mita 120, na anaambiwa unavuna tu, na jengo ni imara linadumu kwa miaka 10 bila matengenezo wala marekebisho.Hizi taarifa huvutia sana watu
B; Ni changamoto zipi wamekutana nazo baadhi ya wakulima wa Green House.
Kwa maeneo ya dar-es-salaam na mikoa mingine zipo baadhi ya green house zimejengwa mwaka jana 2015,lakini wamiliki wake wamezitelekeza na wengine wamezibomoa baada ya.
1.Kuona wanapata mashambulizi mengi ya magonjwa na wadudu.
Wapo baadhi ya wakulima kwa kupata taarifa zisizo sahihi waliaminishwa kuwa hakuna magonjwa wala wadudu wanaoshambulia mazao yaliyopo ndani ya green house.
Hivyo wakulima wakarelax,mawazo yao yakawa ni juu ya mapato ya tani 60.
Matokeo yake wamejikuta wanapata magonjwa na wadudu kama mazao ya shamba wazi.
Unakuta ni green house ya nyanya lakini ndani unakuta kuna shida ya mdudu kama kanitangaze, kuna shida ya nyanya kuoza katika kitako (Blosom end rot)etc.
Unakuta mazao yaliyomo ndani ya green house yana afya mbaya kuliko hata ya yale yaliyopo katika shamba wazi (Open field).
Zipo baadhi ya green house zimetelekezwa na wamiliki wake.
2. Wapo baadhi ya wakulima mazao yao yamenyauka na kufa yakiwa ndani ya green house.
Kuna wakulima walijenga green house kwa matumaini ya kupata pesa ya haraka, na wameishia kupata hasara kwa kuwa hawakupata ushauri sahihi, na mazao yao yamekauka pia kama vile yapo shamba wazi. Green house hizi unakuta ziko eneo la joto kubwa,na kimo cha green house ni chini ya mita 2.5 (Gutter height), na hivyo kufanya joto kuwa kali sana na mazao kunyauka.
Unakuta green house iliyojengwa Mufindi au lushoto, inafananana kimo na ile iliyojengwa dar-es-salaam/Morogoro.
3. Mavuno kidogo.
Wapo wakulima waliolima ndani ya green house, mbali ya kwamba walikuwa wakiaminishwa kuwa watapata mavuno mengi yatakayowafanya kurudisha gharama zao ndani ya msimu mmoja (siku 90-120), matokeo yake imekuwa kinyume kabisa (mavuno hafifu na yasiyo bora)
4.Mavuno kukosa soko.
Baadhi ya wakulima walio na hizi green house waliaminishwa kuwa kwa kuwa ni mavuno ya green house, basi yatapata soko zuri muda wowote atakaovuna.
Kwa sababu hizo wakulima wamezaisha bila hofu, lakini ulipofika wakati wa mavuno imekuwa kilio, bado mazao hayo yamepata bei sawa na yale ya shamba wazi (Open field) na wakati mwingine mazao yao yameharibika kwa kukosa soko.
5.Mazao kuwa SI mazuri, na kutofanana hatua zote za ukuaji.
Baadhi ya wakulima waliaminishwa kuwa mazao yote yaliyomo ndani ya green house yatakuwa katika level moja na yatafanana kwa kuwa yapo katika mazingira mazuri ya aina moja, hivyo kumfanya mmiliki kuamini kuwa kwa kuwa ni green house ni lazima ukuaji uwe bora na mzuri, hata kama hatofanya jitihada zozote, yeye atasubiri kuvuna na kupata pesa tu.
YAPO MENGI YA KUZINGATIA KABLA YA KUINGIA KATIKA KILIMO CHA GREEN HOUSE-BAADHI NI HAYA.
1. ILI UFANIKIWE LAZIMA UWEKE JUHUDI, UMAKINI NA MALENGO KATIKA JAMBO HUSIKA, UNAWEZA KUWA NA GREEN HOUSE NA BADO UKAPATA HASARA KUBWA KULIKO HATA ALIYELIMA OPEN FEILD (SHAMBA WAZI)
2.FAHAMU KILIMO NI SOKO HURIA, USIPOKUWA MAKINI UTAKUTANA NA MAFUNDI FEKI, MBEGU FEKI, MADAWA FEKI, TAARIFA FEKI… MWISHO NI HASARA.
Hivyo niwaombe ndugu zangu tuwe waangalifu sana kwa kila jambo tunalotaka kufanya
3. BINAFSI NAWASHAURI KABLA YA KUANZA KILIMO CHA GREEN HOUSE, NI VYEMA UKAFANYA UTAFITI KIDOGO HASA KUTEMBELEA WALIOFANIKIWA NA PIA SI MBAYA UKAPRACTICE KWANZA KILIMO CHA SHAMBA WAZI (OPEN FIELD) ILI UJUE CHANGAMOTO ZA MAZAO HAYO (WADUDU, MAGONJWA, GHARAMA ETC), KWASABABU USIPOKUWA MAKINI CHANGAMOTO HIZO HIZO ZA SHAMBA WAZI ZITAKUKUMBUKA PIA HATA KAMA UNA GREEN HOUSE.
4. FANYA UTAFITI WA KINA KABLA YA KUAMUA KUINGIA KATIKA KILIMO, JUA NI WAKATI GANI SAHIHI WA KUZALISHA ZAO LAKO (SOKO=JUA SOKO KWANZA KABLA YA KUZALISHA MAZAO YAKO),
5. JUA GHARAMA ZOTE ZITAKAZO KUKABILI NA UJIANDAE, NA JITAHIDI SANA UPATE KWANZA ELIMU/MAHITAJI YA ZAO HUSIKA UNALOTAKA KUZALISHA, ILI UJIANDAE VYEMA NA BAADAE UWEZE KULISIMAMIA VIZURI.
6.HAKIKISHA UNAPATA FUNDI MZOEFU WA UJENZI WA GREEN HOUSE JITAHIDI KWANZA UJIRIDHISHE JUU YA UBORA WA KAZI ZAKE.
By AFO MPELA
http://mpelaaccess.blogspot.com
yohanampela34@gmail.com
KWA USHAURI
+255652535637